MALIGHAFI ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWAAJILI YA UTENGENEZAJI WA BARAKOA AINA YA N95, FFP2 NA ZA UPASUAJI.

Dr. Timo J.C. Oude Vrielink, Prof. Johanna H. Meijer
Idara ya Teknolojia ya Matibabu (Medical Technology) Idara Cell and Chemical Biology
Chuo kikuu cha Tiba cha Leiden, Leiden, Uholanzi

Translated to Kiswahili by Dr. Jeremia J Pyuza
Department of Pathology
Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC), Moshi, Tanzania

Huu ni muhtasari wa chapisho la kisayansi lililochapwa katika Jarida la PLOS ONE; Kwa maelezo zaidi angalia tovuti ifuatayo https://journals.plos.org/plosone/article?id=10.1371/journal.pone.0236239

MAELEZO YA AWALI

Halyard Quickcheck H300- Ni aina ya malighafi, zinazofanana kabisa na nguo ambazo zinatumika kwa kiasi kikubwa kufunika vifaa ya upasuaji wakati wa kuvitakasa(Sterilization) kabla ya vifaa hivyo kutumika kwa ajili ya upasuaji na kufunika wagonjwa (Ona picha hapo chini). Malighafi hizi zinafanana Kabisa na kitambaa, lakini zinaweza kutumika kama mbadala wa malighafi zinazotumika kutengeneza barakoa aina ya FFP2, N95, na zile za upasuaji(Surgical mask).

MUHTASARI

Kutokana na upungufu wa barakoa uliopo sasa uliosababisha ukosefu wa vifaa kinga kwaajili ya watumishi wa afya, Tumetafuta suluhisho/uwezekano utakaowezesha hospitali Kutengeneza barakoa ambazo:

1. Zina vigezo vinavyotakiwa na ubora katika kuzuia/kuchuja vimelea vya magonjwa
2. Ni rahisi kutengenezwa kwa haraka, katika mazingira husika
3. Zinaweza kutengenezwa kwa kutumia malighafi zilizopo na zinazopatikana kiurahisi katika hospitali zote duniani.

Kwa kuwa virusi vinavyosababisha Corona (SARS-CoV-2) huambukizwa kupitia majimaji kutoka katika mfumo wa upumuaji, uhitaji wa barakoa zenye ubora wa hali ya juu, na zilizothibitishwa umeongezeka kwa kasi kubwa. Shirika la Afya Duniani (WHO) limeweka muongozo kuwa watumishi wote wa afya wanaofanya kazi katika vitengo vya wagonjwa mahututi wanapaswa kuvaa barakoa ambazo zina uwezo wa kuzuia/kuchuja angalau asilimia 94% (FFP2) au asilimia 95% (N95) ya vimelea vya magonjwa .

Shirika la Afya Duniani, pia linashauri watumishi wote wa afya kuvaa barakoa za upasuaji (surgical mask), ambazo zina uwezo mkubwa wa kuzuia maji maji machafu mfano,mate,makamasi, damu zinaporuka usoni, lakini zenye uwezo mdogo wa kuzuia/kuchuja chembechembe ndogo mfano vimelea vya magonjwa (Virusi).

Tumefanya utafiti kuona kama malighafi zinazotumika kufungia vifaa ya upasuaji wakati wa utakasaji( sterilization), zinaweza kutumika katika utengenezaji wa barakoa zinazofanana Kabisa na FFP2 yenye uwezo wa kuzuia vimelea vya magonjwa kwa zaidi ya asilimia 94%, N95 zinazoweza kuzuia vimelea vya magonjwa kwa zaidi ya asilimia 95,na barakoa za upasuaji. Malighafi hizi zinazojulikana kama Halyard Quickcheck H300 na zinazalishwa na kampuni ya Owen na Minor, kwa sasa zinatumika  katika hospitali duniani kote kwa ajili ya kufungia vifaa ya upasuaji wakati wa utakasaji( sterilization).

Utafiti wetu ulionesha kuwa, malighafi zinazotumika kwa ajili ya kufungia vifaa vya upasuaji wakati wa utakasaji(Sterilization) zinakidhi viwango vya kuzuia/kuchuja vimelea vya magonjwa ( Tazama Jedwali la 1 hapo chini). Malighafi zilizotengenezwa kwa ubora wa kuta/matabaka/(Layers) matatu zilikuwa na uwezo wa kuzuia/kuchuja kwa kiwango cha asilimia 94,99,na 100 kwa chembe chembe( Particles) zenye ukubwa wa µm 0.3, µm 0.5 na µm 3.0 katika mfululizo uliooneshwa katika asilimia hapo juu. Takwimu hizi za ubora zinakaribiana kabisa na zile ambazo tunazipata tunapotumia aina za barakoa zinazojulikana kama FFP2 na N95.

Malighafi hizi zilipotengenezwa kwa utaratibu wa  matabaka/ kuta mbili,  uchujaji wa chembe chembe ulikuwa 86.60±1.91% kwa chembechembe zenye ukubwa µm 0.3, 98.02±0.46% kwa chembechembe zenye ukubwa wa µm 0.5 µm na 99.97±0.01% kwa chembechembe zenye ukubwa wa µm 5, kiwango ambacho kinafanana na barakoa aina ya FFP1. Pale tulipotumia kuta/tabaka moja tu kwa malighafi hii ubora wake ulifanana na  ule wa barakoa za upasuaji (surgical mask). Hata baada ya kurudia zoezi la utakasaji (Stelization) wa malighafi aina ya halyard H300, bado ubora wake  ulifanana na ule wa barakoa ya upasuaji(Surgical Mask).

Jedwali 1. Uwezo wa kufanya kazi wa Barakoa zilizotengenezwa na Halyard H300 (Quickcheck H300) ukilinganishwa na aina mbalimbali za barakoa zinazotumika kwa sasa( FFP2,N95,na Barakoa za upasuaji(surgical masks)).

 µm 0.3µm 0.5µm  3.0
Barakoa ya upasuaji54.52±2.77%88.61±1.13%98.92±0.64%
Kuta/tabaka 1 H30070.08±0.48%89.68±0.70%99.74±0.13%
Barakoa ya FFP294.08±0.42%99.57±0.04%100.00±0.00%
Kuta/tabaka 3 H30093.84±0.37%99.45±0.08%99.99±0.01%

Tulifanikiwa kutengeneza barakoa iliyokamilika kama mfano ili kuwezesha utengenezwaji wa barakoa katika mazingira ya hospitali husika. Tulikusanya vifaa vya muhimu vinavyohitajika ikiwemo (Aluminum, Mpira aina ya neoprene, na vifaa vyenye kuvutika (elastic) ambavyo vilikuwa na ubora na uhitaji uliohitajika kama ilivyoainishwa katika mchoro namba 1 hapa chini.  Hospitali nyingi hata zile zilizoko sehemu za vijijini vifaa hivi huweza kupatikana.

Kifaa cha muhimu zaidi katika utengenezaji na mtindo tulioutumia ilikuwa mashine ya kukatia aluminium na kamba ndogo ndogo zenye kuvutika. Mtindo tunaoushauri ni rahisi katika utekelezaji, na barakoa tuliyotengeneza ina uwezo wa kumsaidia mtumiaji kupumua vizuri,na kuweza kutumia eneo lote la  barakoa katika kupumua. Hii itamfanya mtumiaji kupumua bila shida na kuwa katika hali ya utulivu anapotumia barakoa hii.

Utafiti huu ulilenga hasa katika kuleta utatuzi wa changamoto ya utengenezaji wa barakoa katika hospitali na mazingira mengine yeyote muhimu yenye uhitaji. Malighafi aina ya Halyard zinazotumika katika kutakasa vifaa  vya upasuaji, zinakidhi vigezo vinavyoshauriwa na Shirika la Afya Duniani,katika kutengeneza barakoa na hivyo barakoa zitokanazo na malighafi hizi, zinaweza kutumiwa na watumishi wa afya katika kujikinga na virusi aina ya SARS-CO-2 hasa kwa watumishi ambao hawawezi kupata barakoa za kununua au hawawezi kununua .

Mchoro 1. Muundo wa barakoa zinazoweza kutengenezwa kwa kutumia malighafi za kufungia vifaa vya upasuaji wakati wa kuvitakasa(Sterilization) katika mazingira ya hospitali. (A) Namna ya kukunja na kushona barakoa (B) Namna ya kuunganisha kifunga pua na sehemu nyingine ya barakoa. Maelezo yaliyo kamili yanapatikana katika jarida ambalo limeshachapishwa,katika tofuti ifuatayo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *